Klabu ya Burnley imeshuka daraja kutoka Premier League baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo uliopigwa nyumbani, matokeo yaliyowathibitishia kushindwa kubaki ligi kuu msimu huu.
Goli pekee la mchezo lilifungwa na nyota wa Manchester City Erling Haaland katika kipindi cha kwanza, likiwapa ushindi muhimu timu ya kocha Pep Guardiola ambayo inaendelea kuwania ubingwa wa ligi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Matokeo hayo yameifanya Burnley kubaki na pointi 20 pekee huku zikiwa zimesalia mechi nne, idadi ambayo haiwezi kuwatosha kufikia nafasi ya salama kwenye msimamo wa ligi. Timu hiyo sasa iko nyuma kwa pointi 13 kutoka eneo la usalama.

Kocha wa Burnley Scott Parker alisema baada ya mchezo “Ni maumivu makubwa kushuka daraja, lakini lazima tukubali hali na kujipanga upya kwa msimu ujao.”
Hii ni mara ya tano mfululizo kwa Burnley kushuka au kupanda daraja, hali inayoonesha mzunguko mgumu wa klabu hiyo kati ya Premier League na Championship, huku kiwango chao kikiwa hakijaimarika kwa muda mrefu kwenye ligi kuu.



