Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeweka wazi kuwa hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwenye timu ya waamuzi wa mchezo wa kwanza wa fainali ya CAF Champions League mjini Pretoria, huku refa Jean Ndala akiendelea kupewa jukumu la kuchezesha pambano hilo licha ya mabishano makubwa yaliyoibuka kuhusu uteuzi wake.

Uamuzi huo umekuja baada ya taarifa kusambaa zikidai kuwa kulikuwa na malalamiko na petition mbalimbali zilizowasilishwa CAF kupinga Ndala kutokana na baadhi ya maamuzi yake yaliyowahi kuzua utata kwenye michuano ya AFCON. Mashabiki na wadau wa soka walionyesha mashaka kuhusu uwezo wake wa kusimamia mechi yenye uzito mkubwa kama hiyo.
Hata hivyo, CAF imesisitiza kuwa ilipitia malalamiko yote yaliyowasilishwa na kuamua kuyatupilia mbali. Kwa mujibu wa shirikisho hilo, hakuna sababu ya kufanya mabadiliko kwani bado wana imani kamili na waamuzi waliopangwa kwa mchezo huo mkubwa wa bara Afrika.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hatua hiyo imeongeza joto kuelekea fainali hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa, huku mijadala ikiendelea mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuhusu kama Ndala ataweza kuhimili presha ya mchezo huo mkubwa bila kuibua mabishano mapya.

Kwa sasa, macho ya mashabiki wa soka Afrika yanaelekezwa Pretoria kusubiri kuona kama refa huyo ataweza kuandika historia nzuri au kuongeza ukurasa mwingine wa mijadala kwenye soka la Afrika. Mechi bado haijaanza, lakini tayari presha imeanza nje ya uwanja.



