Timu za Taifa za Canada na Afrika Kusini zimeandika historia mpya katika soka lao baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya 32 bora ya mashindano ya Dunia 2026 kwa mara ya kwanza tangu zianze kushiriki mashindano hayo. Mafanikio hayo yamekuja baada ya timu hizo kumaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi yao na kujihakikishia tiketi ya hatua ya mtoano.
Afrika Kusini, ambayo ilianza kushiriki fainali za michuano ya Dunia mwaka 1998 nchini Ufaransa, imefanikiwa kuvuka hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika historia yake. Kabla ya mafanikio hayo, Bafana Bafana walishiriki pia michuano ya mwaka 2002 nchini Korea Kusini na Japan pamoja na ile ya mwaka 2010 walipokuwa wenyeji, lakini walishindwa kufuzu hatua ya mtoano.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Hatimaye tumefanikisha jambo ambalo vizazi vingi vya wachezaji wa Afrika Kusini vilikuwa vikilifuatilia kwa miaka mingi,” imeelezwa baada ya timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili Kundi A ikiwa na pointi nne. Matokeo hayo yameifanya Afrika Kusini kuandika ukurasa mpya katika historia ya soka la nchi hiyo.
Kwa upande wa Canada, safari yao yamichuano ya Dunia ilianza mwaka 1986 nchini Mexico ambapo walipangwa Kundi C pamoja na Urusi, Hungary na Ufaransa. Katika ushiriki huo wa kwanza walipoteza michezo yote mitatu na kufungwa mabao matano bila ya kufunga hata moja. Walirejea tena mwaka 2022 nchini Qatar baada ya miaka 36, lakini pia walishindwa kuvuka hatua ya makundi.
“Michuano ya Dunia la 2026 limekuwa la kipekee kwa Canada na Afrika Kusini, kwani limefuta historia ya kushindwa kwa miaka mingi,” amesema mmoja wa wachambuzi wa soka. Canada, ambao ni mmoja wa wenyeji wa mashindano hayo pamoja na Marekani na Mexico, walimaliza nafasi ya pili Kundi B kwa pointi nne na kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika historia yao.


