Klabu ya Manchester United imemtangaza rasmi Michael Carrick kuwa kocha mkuu wa kudumu wa timu hiyo baada ya kufanya vizuri katika kipindi chake cha ukocha wa muda tangu Januari mwaka huu.
Carrick, ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa United kwa miaka kadhaa, alipewa jukumu la kuiongoza timu hiyo kufuatia kuondoka kwa Ruben Amorim, ambapo alianza kwa ushindi mkubwa wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City kabla ya kuibuka na ushindi mwingine wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya Arsenal.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika kipindi chake cha miezi mitano, Carrick pia aliiongoza United kupata ushindi dhidi ya Liverpool, Chelsea, Aston Villa na Tottenham Hotspur, hatua iliyosaidia timu hiyo kupanda kutoka nafasi ya saba hadi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na kufuzu kushiriki michuano ya UEFA Champions League msimu ujao.

Kupitia taarifa rasmi ya klabu hiyo, Manchester United ilithibitisha kuwa Carrick amesaini mkataba mpya utakaomuweka Old Trafford hadi mwaka 2028. Akizungumza baada ya uteuzi huo, Carrick alisema “Tangu nilipowasili hapa miaka 20 iliyopita, nilihisi ukubwa na heshima ya Manchester United. Kupewa jukumu la kuiongoza klabu hii maalum ni fahari kubwa kwangu. Wachezaji wameonyesha moyo mkubwa wa kupambana, umoja na kujituma, sasa ni wakati wa kusonga mbele pamoja kwa malengo makubwa.”



