Manchester United imethibitisha kuwa Casemiro atavaa jezi namba 18 na kufuata nyayo za gwiji wa klabu hiyo Paul Scholes.

Kiungo huyo wa kati wa Brazil, (30), amesajiliwa na Man UTD kwa uhamisho wa paundi milioni 70 kutoka Real Madrid.

casemiro, Casemiro Kufuata Nyayo za Paul Scholes., Meridianbet

Anawasili kama mshindi mara tano wa Ligi ya Mabingwa na moja kati ya viungo wa Ulaya waliofanikiwa zaidi katika muongo uliopita. Lakini nambari yake ya shati ina uzito mkubwa zaidi wa matarajio Old Trafford.

casemiro, Casemiro Kufuata Nyayo za Paul Scholes., Meridianbet

Jezi nambari 18 ilipewa umaarufu na Scholes, ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa katika historia ya Ligi Kuu. Scholes alishinda mataji 11 ya ligi katika kipindi cha miaka 22 cha maisha yake akiwa na Man UTD, na kucheza zaidi ya mechi 700 katika vipindi viwili tofauti vya klabu hiyo.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa