Mchezaji mpya kwenye kikosi cha Manchester united Carlos Henrique Casimiro ameweka wazi sababu iliyomfanya avutiwe kujiunga na klabu hiyo ni kuwa anahitaji kushinda ligi kuu akiwa kwenye viunga vya Old Traford.

Casemiro leo kwenye hafla yake ya kuagwa iliyoandaliwa na klabu ya Real Madrid, alieleza furaha yake ya kujiunga na klabu hiyo kubwa nchini Uingereza.

casemiro, Casemiro: Nataka Kushinda EPL na Man United, Meridianbet

“Haya mabadiliko ni changamoto kubwa kwangu sasa,” alisema Casemiro. “Nilizungumza na mke wangu siku tatu zilizopita  na mke wangu alisema muangalie mtoto wako wa miaka 18 ambaye anashuku kubwa ya kuhusu mradi wake mpya.

“Najisikia furaha kucheza ligi kuu ya Uingereza. Kama ningeweza, ningecheza mchezo wa leo dhidi ya Liverpool. Ninafuraha sana, ni klabu yenye historia kubwa. itanipasa kufanya kazi kwa juhudi ili kutengeneza jina pale, sijashinda kitu bado.

“Nikiwa Manchester United, kwanza kabisa, ninachotaka ni kubadili jinsi ninavyojikia kuhusu klabu, heshima yangu.

“Kila nilichofanya hapa Madrid, nataka nikakifanye kule pia. Nataka kuwaonesha shauku yangu ya upambanaji, uwezo wa kufanya kazi kwa bidii, mtazamo wangu wa kiuweledi. Nataka kufanya kazi kwa juhudi kila siku kuwaonesha jinsi nilivyo makini .

“Nataka kushinda ubingwa wa ligi kule, najua ni ligi inayovutia.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa