Edinson Cavani ameomba radhi kwa chapisho aliloweka katika Instagram yake ambalo linaweza kuchukuliwa kuwa lenye kukera, ingawa Manchester United inasisitiza kuwa hakuna “nia mbaya” kwa upande wa Muuruguai huyo.

Cavani alikuwa mtu muhimu kwa ushindi wa 3-2 wa United dhidi ya Southampton siku ya Jumapili, akianzisha kufunga Bruno Fernandes na Cavani kufunga mara mbili baada ya kuingia kipindi cha pili.

Cavani Aomba Radhi Kwa Chapisho Lake la Instagram.
Cavani akisherehekea goli

Kwa kufanya hivyo, alikua mchezaji wa kwanza tangu bosi wa United Ole Gunnar Solskjaer achukue mikoba ya kuinoa Man United kuhusika kwenye magoli matatu ya Ligi Kuu katika mchezo mmoja baada ya kutoka benchi.

Lakini baada ya mechi alijiingiza kwenye matatizo kwa kuweka post kwenye Instagram yake – ambayo ilifutwa haraka – ambayo alitumia maandishi ya Kihispania ambayo yanaweza kuonekana kuwa ya kijinga wakati akimshukuru rafiki yake.

Chama cha Soka (FA) kiliarifiwa na kuanza kuangalia suala hilo siku ya Jumatatu, lakini Cavani aliomba msamaha masaa machache baadaye.

Katika taarifa iliyotolewa na United, Cavani alisema: “Ujumbe niliochapisha baada ya mechi Jumapili ulikusudiwa kama salamu ya mapenzi kwa rafiki, kumshukuru kwa pongezi zake baada ya mchezo.

“Kitu cha mwisho nilichotaka kufanya si kusababisha ubaya kwa mtu yeyote. Mimi napingana kabisa na ubaguzi wa rangi na nilifuta ujumbe mara tu ilipoelezwa kuwa inaweza kutafsiriwa tofauti.

“Ningependa kuomba msamaha kwa dhati kwa hili.”

Katika taarifa yao wenyewe, United iliongeza: “Ni wazi kwetu kwamba hakukuwa na nia yoyote mbaya nyuma ya ujumbe wa Edinson na akaufuta mara tu alipoambiwa kwamba inaweza kutafsiriwa vibaya.

“Edinson ameomba msamaha kwa kosa hilo ingawa hakuwa na nia mbaya. Manchester United na wachezaji wetu wote wamejitolea kikamilifu katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.”


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Cavani, Cavani Aomba Radhi Kwa Chapisho Lake la Instagram., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa