Klabu ya Manchester United imethibitisha kwamba Edinson Cavani hatopatikana kuwakabili Newcastle United siku ya Jumamosi hii ni kutokana na kufuata taratibu za kuzuia maambukizi ya Corona atalazimika kujitenga kwa siku 14 baada ya kuhama akitokea Ufaransa.
Cavani amesaini mkataba na United kwa uhamisho huru siku ya mwisho katika dirisha la usajili lakini kutokana na miongozo iliyowekwa na United Kingdom ya kujikinga na virusi vya Corona inawataka watu kukaa karantini siku 14 baada ya kutua katika ardhi ya taifa hilo.

Mshambuliaji huyo wa Uruguay alikuja moja kwa moja akitokea Ufaransa moja ya nchi ambazo zipo kwenye list, hii inamaanisha aataendelea kufanya mazoezi binafsi akiwa amejitenga tangu ajiunge na klabu hiyo ya Premier League.
Iliripotiwa kuwa Man United walikuwa wakitafuta ufafanuzi kuhusu muda ambao Cavani atakaa Karantini na kwa sasa wamethibitisha kuwa Cavani, 33 hatoweza kusafiri mpaka Newcastle siku ya Jumamosi.
Maelezo ya United yalisomeka kama hivi kwenye tovuti yao: “Cavani amelazimika kujitenga kutokana na miongozo iliyowekwa kwaajili ya kujikinga na COVID-19, baada ya kutua nchini akitokea Ufaransa, hii inamaanisha hatoweza kucheza mchezo wake wa kwanza katika dimba la St James Park.
Mechi ya kwanza ya Cavani kwa Man United ni kama itakuwa dhidi ya klabu aliyotokea Paris Saint-Germain, ambako alitumia miaka 7 na kuwa mfungaji bora wa muda wote.
Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua.



magdalena
tahadhali ni muhimu kuliko tiba bora achunguzwe kwanza afya yake ili asije kuwa chachu ya wengine kupata maambukizi
Angelina
Corona imeharibu kila kitu
Nasra
Corona hatari
Dorophina
Pole yake
Shani
Corona ni hatari sana kwenye michezo
Sauda
Pole sana
jullie
pole yake
Genia Sikaluzwe
Pole yake
Adelta
Pole yake
Ernest
Sio mbaya Cavani atapata muda muda mwingi kuangalia viwango na aina ya uchezaji kwa wachezaji wenzake kabla hajaingia vitani rasmi
Issa
Game poa
Mwanahamisi
Corona sio poa
Amiri Kayera
Duh x tunatak kuon Moto wake
Ester mmakasa
Ni vizuri kwa sababu ya tahadhari kwake na wachezaji wenzake.
aisha
Game kalii
Caroline
Corona inavuruga mambo
Mwajumah
Pole yake
Janeflora malisa
Pole
Fatuma kasomo
Polee sana
Saupha mohamed
Pole yake
Sabrina
Duuh Corona ni changamoto kubwa kwenye tathinia ya michezo
Povel
Duh cavani hatapat nafas ya kuangaliah mchezo na kujifunza wenzak jinsi wanavyochezah na kugain ustad na mapunguf ya wenzake
Gabriel
achunguzwe kwanza afya yake ili asije kuwa chachu ya wengine kupata maambukizi
latifa juma mohamed
Pole yake.
Tatu
Corona sio poa
Hopemwaikuka
🙌