KATIKA kuhakikisha kuwa wanatetea ubingwa wa ligi kuu benchi la ufundi la klabu ya Yanga limeweka wazi mipango yao ya kuhakikisha kuwa wanapata ushindi mnono katika michezo yao ya nyumbani baada ya kumaliza ile ya ugenini kwa ushindi.
Kaze : Azam FC Walistahili Kutinga Fainali.
Cedric Kaze

Yanga imefanikiwa kucheza mizhezo miwili ya ugenini ambapo ilifanikiwa kucheza dhidi ya Polisi Tanzania na kushinda 2-1 kabla ya kucheza na Coastal Union ambapo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Cedric Kaze Kocha msaidizi wa Yanga alisema kuwa mara baada ya kushinda ugenini kwa sasa nalengo yapo ni kuhakikiha kuwa wanaibuka na ushindi mnono katika michezo ya nyumbani inayofuata ili kuhakikisha wanarejea kileleni kwaajili ya mpango wao wa kuutetea ubingwa wao.
Cedrick kaze
Cedric kaze

“Michezo ya ugenini ilikuwa ni migumu sana kwa upande wetu na tunachoshukuru ni kuweza kupaata matokeo katika michezo hiyo ambapo kwasasa jambo kubwa kwetu ni kuhakikisha kuwa michezo inayofuata amabayo tutacheza nyumbani katika viwanaja vizuri ni tufanikiwe kushinda ushindi wa ishindo.

“Yanga hatujaridhika kiasi cha kusema kuwa tusiendelee kutaka kupata mafanikio mengine kwa msimu huu,malengo yetu ni lazima tufanikiwe kuutetea ubingwa wetu na ndipo tunapoelekea kwa sasa ambapo lazima tuhakikishe kuwa tunatwa ubingwa wa msimu huu,”alisema kocha huyo.

Yanga katika mchezo unaofuata wa ligi kuu wanatarajiwa kukipiga dhidi ya Azam FC katika mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Mkapa Dar.


Kwa taarifa za kimichezo na uchambuzi sasa unaweza kutazama video hizo kwa kupitia youtube . USISAHAU KU SUBSCRIBE

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa