Baada ya Yanga kumtambulisha Andre Mtine kama Mtendaji Mkuu wao mpya nimepitia vyanzo mbalimbali vimeonesha kuwa ana rekodi za kesi na tuhuma mbalimbali.

CEO Andre Mtine
CEO Andre Mtine

1- KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA (2007) NDOLA, ZAMBIA

– Andre Mtine alikamatwa na Mamlaka nchini Zambia kutokana na sakata la utakatishaji fedha wa kiasi na wizi wa kiasi cha Kwacha Million 100 sambamba na Maofisa wawili waandamizi ndani ya benki ya Posta ya Zambia.

Wahusika walikuwa Mtine, 43, a Football Association of Zambia (FAZ) Finance manager, Gilbert Kapambwe, 42 na Financial accountant Ignatius Kapembwa.

2- KUKAMATWA NA MAMLAKA ZA UHAMIAJI ZAMBIA 🇿🇲 2013

Mtine alikamatwa na Mamlaka za Uhamiaji nchini Zambia mnamo tarehe 18- 10- 2013 majira ya saa 6:30 mchana kutokana na kuvunja sheria za Uhamiaji kwa wachezaji watatu Stopilla Sunzu, Nathan Sinkala na Reinford Kalaba ambapo baadae waliitwa kutoa maelezo na wakaachiwa.

CEO Andre Mtine
CEO Andre Mtine

3- KUKAMATWA NA MAMLAKA KUHUSU WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA ZAMBIA 🇿🇲 (2014)

Ceo huyo inasemekana alishawishi wachezaji Nathan Sinkala na Stopilla wasusie mechi ya timu ya taifa ya Zambia dhidi ya Japan, huku pia FAZ wakisema wazi yeye ndie chanzo cha mgogoro kati yao na klabu ya TP Mazembe.

Alifungiwa maisha kujihusisha na soka nchini Zambia.


Kwa video za kimichezo na uchambuzi Tembelea Meridianbet Sport Youtube au gusa Video hii kutazama video nyingi zaidi, USISAHAU KU SUBSCRIBE

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa