Klabu ya Chelsea inatarajia kumsajili beki wa kati wa RB Leipzig Josko Gvardiol majira ya msimu wa joto wa 2023. Klabu imewasilisha ombi kwa Leipzig karibu €90M kwaajili ya kumpata beki huyo.

Beki huyo angesalia Leipzig msimu huu kwani hawakutaka kumuuza, hivyo angejiunga na Chelsea mnamo Juni 2023. Mazungumzo bado yanaendelea kwa vilabu na upande wa wachezaji kujaribu kufikia makubaliano kabla ya dirisha kuisha.

Chelsea Kumsajili Josko Gvardiol.

Vilevile inaelezwa kuwa klabu ya Manchester City nao wamekuwa wakimtaka kumsajili mchezaji huyo lakini kwasasa wameelekeza nguvu zao kwa Manuel Akanji kama dili la dakika za mwisho,ambalo linatarajia kukamilika kwa €17M.

Chelsea Kumsajili Josko Gvardiol.

Chelsea mpaka sasa wanapitia wakati mgumu sana kutokana na kutokuwa na matokeo ambayo wanayapata, hata hivyo kukosekana kwa baadhi ya wachezaji imeweza kuchangia mfano Ngolo Kante katika eneo la kiungo, kuuzwa na kutolewa kwa mkopo baadhi ya wachezaji hasa katika eneo la ushambuliaji na kutonunua wengine katika eneo hilo pia.

Mpaka sasa  Chelsea ipo katika nafasi ya 8 katika msimamo huku akiwa ameshinda mechi mbili, sare moja , huku akiwa hajaruhusu goli katika mechi moja, kapoteza mechi mbili  na zote zikiwa za ugenini ambazo ni dhidi ya Leeds United, na Southhampton.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa