Klabu ya Chelsea ipo karibu kumsajili beki wa kati Kalidou Koulibaly kutoka Napoli kwa kitita cha pauni milioni 33.7 ambapo kwa sasa wanajaribu kujenga safu ya ulinzi kufuatia kuondoka kwa Rudiger na Christensen.

Koulibaly tayari amefanya makubaliano binafsi na Chelsea Koulibaly atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Chelsea baada ya kumsajili Raheem Sterling kutoka Manchester City kwa dili ya miaka mitano mapema wiki hii na siku ya Alhamisi alikuwa akiwaaga mashabiki wa City.

Ingawa kocha wa Napoli Luciano Spaletti alidai kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal hadhani kama ataondoka wakati wa dirisha hili la usajili kwani ndiye mchezaji wao muhimu na anatizamia kumpa unahodha kwa msimu ujao lakini kama Kalidou akiamua kuondoka watamshukuru pia.

Pamoja na kwamba Chelsea wamekamilisha baadhi ya sajili lakini bado Tuchel anataka kuongeza wachezaji kwenye kikosi chake kuelekea kwa msimu mpya.


BASHIRI HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa