Chelsea FC ni klabu ya mpira wa miguu ya nchini Uingereza iliyo na maskani yake Fulham, London.

Klabu hii ilianzishwa mwaka 1905, na kwa miaka mingi sana imekuwa ikishiriki ligi kuu ya Uingereza. Uwanja wao wa nyumbani ni Stamford Bridge ambao una uwezo wa kuingiza watazamaji 41,837, wameutumia uwanja huu tangu klabu ilivyoanzishwa.

Chelsea, kwa mara ya kwanza ilipata mafanikio makubwa mwaka 1955, ambapo walipata ubingwa wa ligi, na walishinda mataji kadhaa katika miaka ya 1960, 1970, 1990 na 2000. Klabu hii imefurahia zaidi mafanikio katika miongo miwili ilopita, kwa kushinda mataji makubwa 15 tangu mwaka 1997.

Chelsea Wanafikisha Mchezo wa 1,000 Wikendi hii.
Wachezaji wa Chelsea wakisherehekea baada ya kushinda ubingwa wa Ulaya mwaka 2012.

Nyumbani, Chelsea imeshinda ubingwa wa ligi mara nne, kombe la FA mara saba, kombe la ligi mara nne, pamoja na ngao za jamii mara nne. Na kimataifa Chelsea imeshashinda UEFA Cup Winners’ Cups mara mbili, UEFA Super Cup moja, UEFA Europa League moja na UEFA Champions League moja.

Chelsea ndio klabu pekee kutoka London kushinda UEFA Champions League, na ni moja kati ya klabu nne kutoka Uingereza, kuchukua makombe yote makubwa matatu ya Ulaya.

Kwa kawaida Chelsea huvaa jezi ya blu, kaptula blu na soksi nyeupe. Nembo ya klabu imebadilishwa mara nyingi kulingana na wakati na kuboresha muonekano wa klabu. Nembo ya sasa inaonesha picha ya simba akiwa amebeba mkuki. Tangu Julai 2003, Chelsea imekuwa ikimilikiwa na Bilionea wa Kirusi, Roman Abramovich.

Vijana wa Frank Lampard watashuka dimbani siku ya Jumapili kuumana na vijana wa Jose Mourinho katika dimba la Stamford Bridge na utakuwa ni mchezo wa 1,000  kwa timu ya Chelsea.

Takwimu za Chelsea chini ya Roman Abramovich:

Mechi – 999.

Ushindi – 608.

Sare – 215.

Kupoteza – 176.

Mataji – 18.

Pesa iliyotumika katika sajili tangu Abramovic aichukue Chelsea inakadiriwa kufika £2bn.

Wastani wa ushindi 61%.

kushinda taji kila baada ya michezo 55.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa