Matajiri wa London Chelsea wamemtangaza Laurence Stewart kuwa mkurugenzi wa ufundi akiwa na jukumu la kusimamia mpango wa mtindo wa vilabu vingi akitokea katika klabu ya Monaco ya Ligue 1.

Stewart ambaye ni mchambuzi wa zamani wa Uingereza wakati wa kombe la dunia la mwaka 2014  anatarajiwa kutua darajani kwaajili ya kukamilisha dili hiyo.

Chelsea ya Mteua Stewart Kusimamia Mtindo wa Vilabu Vingi

Mtindo wa vilabu vingi ni nini?

Ni mtindo unao ruhusu mmiliki kuwa na umiliki wa vilabu katika mataifa mengine. Hakuna sheria zinazo kataza mmiliki kumiliki klabu moja katika kila nchi, na kwa mujibu wa utafiti wa 2021 na Play The Game, vilabu 15 vya Kiingereza vilikuwa sehemu ya mfumo wa vilabu vingi – zaidi ya nchi yoyote Ulaya.

Stewart ambaye anauzoefu na majukumu ya mtindo huo katika soka la kisasa anaonekana kutua darajani kwaajili ya kurahisisha mipango hiyo mipya ya Chelsea chini ya utawala wa Todd Boehly.

Boehly anashauku ya kuipeleka Chelsea kwenye mtindo huo wa vilabu vingi akizifuata nyayo za Manchester City na The City Football Group ambao wanamiliki timu katika mataifa 11.

“Stewart ni chaguo muhimu kwani tunapanga kujenga timu pana ya michezo ambayo itashirikiana kwa karibu,” Boehly alisema katika taarifa yake na mmiliki mwenzake Behdad Eghbali.

“Ni kiongozi wa soka wa kiwango cha kimataifa ambaye anaelewa usimamizi wa vipaji, data na skauti, ukuaji wa wachezaji na uchezaji.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa