Klabu ya Chelsea FC ina hofu kuwa kushindwa kufuzu michuano ya Ulaya msimu ujao kunaweza kuathiri uwezo wao wa kuvutia wachezaji wakubwa katika dirisha la usajili wa majira ya kiangazi.
Ripoti zinaeleza kuwa Chelsea imeonyesha nia ya kumsajili winga wa Newcastle United, Anthony Gordon, lakini hali ya sasa ya klabu hiyo imeanza kuwa kikwazo kikubwa katika kufanikisha dili hilo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Inaelezwa kuwa Chelsea imefanya mawasiliano ya awali kuhusu uwezekano wa kumpata Gordon ikiwa atapatikana sokoni mwezi Juni, lakini kwa sasa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanaonekana kuongoza katika mbio za kuwania saini yake.
Vyanzo vya karibu na klabu hiyo vinaeleza kuwa ndani ya Stamford Bridge kuna hofu kuwa Chelsea haionekani tena kama sehemu bora kwa nyota wakubwa wa Ulaya kutokana na kukosekana kwa utulivu wa kiushindani na matokeo yasiyoridhisha msimu huu.
“Anthony Gordon kwa sasa haioni Chelsea kama chaguo bora zaidi,” kilieleza chanzo kimoja, kikidai kuwa Bayern Munich wana faida ya kuwa na mfumo thabiti wa kiushindani pamoja na nafasi kubwa ya kupigania mataji makubwa barani Ulaya.
Chelsea kwa sasa ipo nafasi ya tisa katika msimamo wa Premier League na bado haina kocha wa kudumu, huku matumaini yao makubwa yakibaki katika fainali ya FA Cup Final ili kuokoa msimu wao. Taarifa zinaongeza kuwa klabu hiyo inapanga kusajili winga, kiungo, beki wa kati pamoja na mshambuliaji mpya, lakini hali yao ya sasa inaweza kuwa changamoto kubwa katika kushawishi wachezaji wa kiwango cha juu kujiunga nao.


