Klabu ya Chelsea fc imepigwa faini ya pauni milioni 10.75 na kupewa adhabu ya kusimamishwa kusajili wachezaji kwa dirisha moja la usajili ikiwa ni adhabu iliyosimamishwa, kufuatia ukiukwaji wa kihistoria wa kanuni mbalimbali za ligi. Hatua hiyo imetangazwa na EPL kupitia taarifa rasmi.
Katika taarifa hiyo, EPL ilisema imekamilisha michakato miwili tofauti ya kinidhamu dhidi ya Chelsea baada ya klabu hiyo kujiripoti yenyewe kuhusu uwezekano wa ukiukwaji wa baadhi ya kanuni zilizotokea miaka ya nyuma.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa mujibu wa makubaliano ya adhabu yaliyothibitishwa na tume huru ya nidhamu, Chelsea imekubali kulipa jumla ya faini ya pauni milioni 10.75 kwa kukiuka kanuni za ligi zinazohusiana na utoaji wa taarifa za kifedha, uwekezaji wa watu wa tatu pamoja na maendeleo ya wachezaji vijana.
Mbali na faini hiyo, klabu hiyo imeadhibiwa kwa kupigwa marufuku kusajili wachezaji wa akademi kwa kipindi cha miezi tisa kuanzia sasa, huku pia ikipewa adhabu ya kusimamishwa kusajili wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa mwaka mmoja, adhabu ambayo imesimamishwa kwa kipindi cha miaka miwili.
EPL imeeleza kuwa ukiukwaji huo ulifanyika kati ya mwaka 2011 na 2018 wakati klabu hiyo ikimilikiwa na bilionea wa Urusi Roman Abramovich, ambapo malipo kwa watu wa tatu yalifanyika bila kuripotiwa kwa ligi, jambo ambalo lilidaiwa kuipa Chelsea manufaa katika kipindi hicho.


