Christian Eriksen Amesaini Man Utd?

Kiungo wa kimatiafa wa Denmark Christian Eriksen amehusiswha kujiunga na klabu ya Manchester United na kupewa mkataba wa miaka mitatu lakini mpaka sasa hakuna taarifa rasmi zinazosibitisha hilo.

Christian Eriksen mwezi january alisajiriwa na klabu ya Brentford, baada ya kuwa nj’e ya uwanja kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya moyo aliyoyapata akiwa anaitumikia timu yake ya taifa kwenye michuano ya EURO2020.

Awali alikuwa anaichezea klabu ya Inter milan, baada ya kupata matatizo ya moyo na kupandikiziwa kifaa maalum kwa ajiri ya kusaidia mapigo ya moyo,  klabu ya Inter Milan ilibidi isitishe mkataba wake kutokana na sheria za nchini humo kutokuruhusu hilo.

Kulikuwa na taarifa kuwa Eriksen alipewa offer kutoka klabu ya Manchester united na aliikataa, na habari kusambaa kuwa amekataa kujiunga na klabu hiyo.

Christian Eriksen pia amewai kuvichezea vilabu ya Ajax, Tottenham Hotspurs na Inter milan.


 

Acha ujumbe