City Watoa Onyo Kali Dhidi ya Matumizi ya Jina la Mchezaji Wao

Manchester City wametangaza kuwa wanazingatia kuchukua hatua za kisheria kufuatia madai yaliyotolewa na mgombea urais wa Real Madrid, Enrique Riquelme, kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wao nyota Erling Haaland. Klabu hiyo imesema haijaridhishwa na namna jina la mchezaji wao linavyotumika kwenye mijadala ya uhamisho.

City Watoa Onyo Kali Dhidi ya Matumizi ya Jina la Mchezaji WaoKwa mujibu wa madai yaliyotolewa na Riquelme, Haaland ana kipengele maalum kwenye mkataba wake ambacho kinaweza kumruhusu kujiunga na Real Madrid iwapo atachaguliwa kuwa rais wa klabu hiyo. “Haaland ana kifungu maalum kinachoweza kufanikisha uhamisho wake kwenda Bernabéu,” alinukuliwa akidai mgombea huyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hata hivyo, baba wa mchezaji huyo pamoja na mawakala wake wameripotiwa kukanusha taarifa hizo, wakisisitiza kuwa hakuna makubaliano yoyote ya aina hiyo. “Hayo siyo kweli, hakuna kipengele kama hicho kwenye mkataba wake,” ilielezwa kutoka upande wa familia na wasimamizi wa mchezaji huyo.

City Watoa Onyo Kali Dhidi ya Matumizi ya Jina la Mchezaji WaoManchester City nao wametoa tamko rasmi wakipinga uvumi huo, wakieleza kuwa taarifa zilizotolewa kutoka Hispania hazina ukweli. “Taarifa hizi si za kweli, hakuna uwezekano wa jambo hilo kutokea,” ilisema sehemu ya taarifa yao ya klabu.

City Watoa Onyo Kali Dhidi ya Matumizi ya Jina la Mchezaji WaoKlabu hiyo imeongeza kuwa inaweka wazi msimamo wake kuhusu matumizi ya jina na taswira ya mchezaji wao katika mjadala huo, na sasa inafikiria hatua za kisheria. “Hatukubaliani na matumizi ya picha na jina la mchezaji wetu katika muktadha huu, tunafikiria hatua za kisheria,” ilihitimisha taarifa hiyo, huku ikisisitiza kuwa Haaland bado ni sehemu muhimu ya mipango yao ya muda mrefu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.