Uongozi wa Coastal Union FC umefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kusitisha Mkataba na kocha mkuu Mohammed Muya. Katika taarifa kwa umma, klabu imemshukuru mwalimu Muya kwa mchango wake alioutoa kipindi chote alichoiongoza timu.
Taarifa hiyo imesema kuwa uongozi wa Coastal Union utaujulisha umma kuhusu muundo na uongozi mpya wa benchi la ufundi muda mchache ujao.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, klabu inaendelea kukabiliana na changamoto kubwa za ligi, ikiwa sasa ipo nafasi ya 13 ikiwa na alama 16. Nafasi hii inakisia uwezekano wa kushuka daraja au kucheza play-off endapo matokeo mabaya yataendelea.
Coastal Union inashikilia nafasi ya juu kidogo kuliko Fountain Gate (nafasi 14, alama 16), Tanzania Prisons (nafasi 15, alama 13), huku KMC ikiwa wa mwisho ikiwa na alama 8. Wakati wa uongozi wa Muya, timu imekuwa na mwendelezo wa matokeo yasiyoridhisha, jambo lililokuwa changamoto kubwa kwa mashabiki na uongozi Wanamangushi.
Kuondoka kwa Muya kunakuja wakati timu inahitaji mabadiliko haraka ili kuepuka kushuka daraja msimu huu. Uongozi wa klabu umesema kuwa watatangaza kocha mpya katika muda wa karibu na wanatarajia kuimarisha benchi la ufundi na kuiboresha timu.


