Kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Cole Palmer, ameripotiwa kuwa tayari kufikiria uwezekano wa kujiunga na Manchester United, licha ya klabu yake ya sasa kusisitiza kuwa haina mpango wa kumuachia katika dirisha lijalo la usajili.
Palmer amekuwa akikosolewa vikali na mashabiki wa Chelsea msimu huu kutokana na kushuka kwa kiwango chake. Nyota huyo wa kimataifa wa England amefunga mabao manne pekee yasiyo ya penalti katika Ligi Kuu England, jambo lililosababisha baadhi ya wachambuzi kuhoji nafasi yake katika kikosi cha Thomas Tuchel kwa ajili ya Kombe la Dunia.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kiwango chake kibovu kilionekana wazi katika kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Nottingham Forest, ambapo alikosa penalti muhimu akiwa na jezi namba 10 ya Chelsea. Matokeo hayo yaliongeza presha kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.
Hata hivyo, licha ya kushuka kwa hali ya kujiamini, tetesi kuhusu mustakabali wake zimeendelea kushika kasi. Kwa mujibu wa ripoti kutoka Daily Mail, vyanzo vilivyo karibu na mchezaji huyo vimedai kuwa Palmer yuko tayari “kufikiria uhamisho” kwenda Manchester United iwapo nafasi hiyo itajitokeza.
Kwa upande mwingine, vyanzo vya ndani ya Stamford Bridge vimesisitiza msimamo wa klabu hiyo kwa kusema “Tutakataa ofa yoyote itakayowasilishwa. Palmer hauzwi katika dirisha lijalo la usajili.” Kauli hiyo inaonyesha dhamira ya Chelsea kubaki na mchezaji wao muhimu licha ya presha ya nje.
Aidha, Palmer mwenyewe alikariri mwezi Aprili kupitia The Guardian kuwa hana mpango wa kuondoka Chelsea kwa sasa, licha ya kukulia akiwa shabiki wa Manchester United. “Ninachotaka ni kumaliza msimu vizuri na kupigania nafasi yangu katika kikosi cha England,” alisema, akilenga kurejea kwenye kiwango chake bora na kumshawishi Tuchel kumjumuisha katika kikosi cha Kombe la Dunia.


