Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo amechaguliwa kwenye kikosi bora cha mwaka cha ligi kuu ya uingereza PFA akiwa pamoja na wachezaji watatu wa klabu ya Manchester CityJoao Cancelo, Bernardo Silva na Kevin De Bruyne

Cristiano Ronaldo, Ijapokuwa timu ya Manchester United haikufanikiwa kufanya vizuri kwenye msimu uliyoisha, lakini yeye alikuwa na wakati mzuri tokea alivyorejea ndani ya dimba la Old Trafford kwenye usajiri wa majira ya kiangazi yaliopita akitokea Juventus.

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo kwenye msimu wa 2021/22 akiwa na Man Utd amefanikiwa kufunga magoli 18 kwenye ligi kuu, huku akimaliza nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji bora EPL, na pia jumla ya magoli 24 amefunga kwenye michuano yote msimu huu.

Pia klabu ya Liverpool imefanikiwa kutoa wachezaji watano, Man city wachezaji watatu, Man Utd mchezaji mmoja, Chelsea mchezaji mmoja, Arsenal na Tottenham hawakufanikiwa kutoa mchezaji kwenye kikosi cha wachezaji kumi na moja wa kikosi cha kwanza.

PFA Timu Bora ya Mwaka

 1. Alisson (Liverpool)
 2. Trent Alexander-Arnold (Liverpool)
 3. Virgil van Dijk (Liverpool)
 4. Antonio Rudiger (Chelsea)
 5. Joao Cancelo (Man City)
 6. Bernardo Silva (Man City)
 7. Thiago (Liverpool)
 8. Kevin De Bruyne (Man City)
 9. Sadio Mane (Liverpool)
 10. Cristiano Ronaldo (Manchester United)
 11. Mohamed Salah (Liverpool)

ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa