Kocha wa Croatia, Zlatko Dalić, amesema anaamini mchezo wa hatua ya 32 Bora ya michuano ya Dunia dhidi ya Ureno utatawaliwa zaidi na “vita ya viungo wa kati” kuliko mvutano wa nyota wawili Luka Modrić na Cristiano Ronaldo.
Dalić alisema kuwa Ureno ina kiungo imara na timu yenye ubora wa kiufundi, akisisitiza kuwa makosa madogo yatakuwa na gharama kubwa katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu na wa ushindani mkubwa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Ninaamini huu utakuwa mchezo wa vita ya viungo wa kati. Ureno wana wachezaji bora sana eneo hilo na ni timu yenye mbinu nzuri. Katika mchezo huu kila kosa litaadhibiwa,” alisema Dalić.
Croatia imeonyesha uimara wake baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya England lakini ikarejea kwa ushindi dhidi ya Panama na Ghana, huku ikijipanga kuendeleza ubora huo dhidi ya Ureno iliyoonyesha matokeo yasiyo thabiti kwenye hatua ya makundi. “Ni timu inayopenda kumiliki mpira muda wote. Ureno ina mapungufu machache sana na inaweza kusababisha hatari muda wowote,” aliongeza kocha huyo.
Nahodha wa Croatia, kipa Dominik Livaković, alisema mechi hiyo inaweza kuwa ya kihistoria kwa nyota wakongwe Modrić na Ronaldo, akiwataja kama wachezaji waliotoa mchango mkubwa katika soka la dunia.


