Mchezaji wa Tottenham Ben Davies amesaini mkataba mpya na klabun hiyo mpaka 2025 klabu hiyo ya London Kaskazini imethibitisha.

Baada ya Spurs kuwasajili Richarlison, Yves Bissouma na Ivan Perisic sasa imembakisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales ili kuwa na kikosi cha ushindani katika ligi na Ligi ya Mabingwa.

Davies alitua Spurs mwaka 2014 chini ya mwalimu Mauricio Pochettino ambapo amefanikiwa kucheza michezo 271 kwenye mashindano yote.

Tottenham waliandika katika ukurasa wao rasmi wa Twitter: “Tunayofuraha kutangaza kwamba Ben Davies amesaini mkataba mpya na klabu mpaka mwaka 2025.

Davies ambaye ana umri wa miaka 29 amesemahaikuwa kitu kigumu kwa yeye kusaini mkataba mpya na Spurs wakiwa chini ya kocha Antonio Conte.

“Nafurahi kusaini mkataba mpya,” aliiambia tovuti rasmi ya klabu. “Nimekuwa nikifurahi soka na fursa ya kuongeza mkataba mpya, nilikuwa na zaidi ya furaha kufanya hivyo. Hakika ni nyakati nzuri kuwa hapa najihisi kuwa nyumbani.


BASHIRI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa