De la Fuente Aisifu Cape Verde Baada ya Kuizuia Hispania Kwa Sare ya 0-0

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya, Luis de la Fuente, amewataka mashabiki na wadau wa soka kuwa watulivu baada ya timu yake kutoka sare ya bila kufungana (0-0) dhidi ya Cape Verde katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi H wa mashindano ya Dunia 2026.

De la Fuente Aisifu Cape Verde Baada ya Kuizuia Hispania Kwa Sare ya 0-0Licha ya mabingwa hao wa Ulaya kutawala umiliki wa mpira kwa kiasi kikubwa na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga, walishindwa kuzitumia ipasavyo huku Cape Verde ikionyesha uimara mkubwa wa kujilinda na kuwazuia Wahispania kupata bao.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza baada ya mchezo huo, De la Fuente alikiri kuwa timu yake ilikosa umakini na ubunifu wa mwisho mbele ya lango, akisisitiza kuwa wakati mwingine matokeo ya soka huamuliwa na mambo madogo ambayo hayawezi kudhibitiwa.

De la Fuente Aisifu Cape Verde Baada ya Kuizuia Hispania Kwa Sare ya 0-0“Suluhisho ni kuendelea kusisitiza falsafa yetu ya mchezo na kuboresha umaliziaji. Tulitengeneza nafasi nyingi lakini hatukuwa na ubora wa mwisho unaohitajika katika mechi za aina hii,” alisema De la Fuente.

Kocha huyo pia aliisifu Cape Verde kwa mpangilio wake mzuri wa kiuchezaji, akieleza kuwa walijilinda kwa wachezaji wengi nyuma jambo lililowafanya kuwa wagumu kuvunjwa licha ya presha kubwa kutoka Hispania.

De la Fuente Aisifu Cape Verde Baada ya Kuizuia Hispania Kwa Sare ya 0-0“Ni timu iliyopangwa vizuri sana. Walicheza kwa kujilinda kwa kina na hali hiyo ilifanya iwe vigumu kupata nafasi wazi. Hata hivyo tulitengeneza nafasi kadhaa, lakini mpira haukutaka kuingia wavuni,” aliongeza.

De la Fuente Aisifu Cape Verde Baada ya Kuizuia Hispania Kwa Sare ya 0-0Matokeo hayo yanaifanya Hispania kuanza kampeni yao ya mashindano hayo kwa pointi moja, huku De la Fuente akisisitiza kuwa bado wana muda wa kurekebisha makosa na kurejea kwenye kiwango chao katika mechi zijazo za kundi hilo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.