De la Fuente Aisifu Spain Baada ya Ushindi Mgumu Dhidi ya Uruguay

Kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Luis de la Fuente, ameisifu timu yake kwa uimara na ustahimilivu baada ya kuibuka na ushindi mgumu wa bao 1-0 dhidi ya Uruguay katika mashindano ya Dunia 2026, ushindi uliowawezesha kumaliza kileleni mwa Kundi H.

De la Fuente Aisifu Spain Baada ya Ushindi Mgumu Dhidi ya UruguayHispania ilikamilisha hatua ya makundi ikiwa na mabao matano bila kuruhusu bao hata moja, jambo lililoendeleza rekodi yao ya kutopoteza mechi kwa mfululizo wa michezo 34, huku De la Fuente akieleza kuwa hilo ni fahari kubwa kwa kikosi chake.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hata hivyo, mchezo huo uliacha majeraha kwa baadhi ya wachezaji ambapo mshambuliaji Yeremy Pino anahofiwa kupata jeraha la mfupa na huenda akakosa mashindano yaliyosalia, huku Nico Williams akimaliza mchezo akiwa na maumivu madogo.

De la Fuente Aisifu Spain Baada ya Ushindi Mgumu Dhidi ya Uruguay“Tulilazimika kupambana hadi kikomo. Wachezaji wangu walijikuta wakipitia mchezo mgumu sana kimwili, lakini walionyesha moyo wa kupambana,” alisema De la Fuente. Aliongeza kuwa hakutaka kulalamikia waamuzi bali alijikita kwenye juhudi za kikosi chake.

De la Fuente Aisifu Spain Baada ya Ushindi Mgumu Dhidi ya UruguayKocha huyo pia alizungumzia ubora wa kiungo wake akisisitiza kuwa wachezaji kama Pedri, Fabián Ruiz, Dani Olmo, Mikel Merino na Martín Zubimendi wanaweza kubadilishana kulingana na mpinzani, huku akisema eneo la kuboresha ni kasi ya pasi na mzunguko wa mchezo.

De la Fuente Aisifu Spain Baada ya Ushindi Mgumu Dhidi ya Uruguay“Nina imani kubwa na kikosi hiki. Ni timu inayotaka kuendelea kukua. Tuko kwenye njia sahihi, lakini kila mchezo unaokuja utakuwa mgumu zaidi,” alihitimisha kocha huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.