De la Fuente amsifu Merino baada ya kuipeleka Hispania nusu fainali

Kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Luis de la Fuente, amempongeza kiungo Mikel Merino kwa mchango wake mkubwa kama mchezaji wa akiba baada ya kufunga bao la ushindi katika dakika za mwisho na kuiwezesha Hispania kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ubelgiji kwenye robo fainali ya michuano ya Dunia 2026. Katika mchezo huo, Fabian Ruiz, ambaye alianza kikosini badala ya Pedri, alifungua ukurasa wa mabao kabla ya Merino kufunga bao la ushindi dakika mbili baada ya kuingia uwanjani.

De la Fuente amsifu Merino baada ya kuipeleka Hispania nusu fainaliDe la Fuente alisema Merino ameendelea kuthibitisha umuhimu wake kila anapopewa nafasi ya kucheza, licha ya kutokuwa miongoni mwa wanaoanza kikosini. “Si haki kusema Merino hastahili kuanza, lakini pia si haki kumuacha nje mchezaji mwingine. Ni wachezaji 11 tu wanaoweza kuanza, na wote wanaelewa jukumu lao. Wanapoingia uwanjani wanajua wanachopaswa kufanya, ndiyo maana ni furaha kuwa kocha wao,” alisema.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo alisisitiza kuwa mafanikio ya Hispania hayatokani na nyota mmoja bali ushirikiano wa kikosi kizima. Kilicho muhimu ni timu. Haijalishi nani anaanza mchezo, kila mmoja ana nafasi muhimu, hata wale ambao hawajapata dakika za kucheza. Huo ndiyo msingi wa mafanikio yetu,” alieleza.

De la Fuente amsifu Merino baada ya kuipeleka Hispania nusu fainaliAkizungumzia namna anavyodumisha umoja licha ya ushindani mkubwa wa nafasi kikosini, De la Fuente aliwasifu wachezaji wake kwa ukomavu na nidhamu yao. Moja ya nguvu zetu ni kwamba hatuna tu wachezaji bora duniani, bali pia watu bora wenye kuheshimiana. Heshima ndiyo msingi wa kila kitu tunachokifanya, na timu hii ya taifa ni mfano mzuri wa hilo,” alisema.

De la Fuente amsifu Merino baada ya kuipeleka Hispania nusu fainaliBaada ya ushindi huo, Hispania sasa itavaana na Ufaransa katika hatua ya nusu fainali kuwania tiketi ya kucheza fainali. De la Fuente anaamini mchezo huo utakuwa mgumu lakini ana imani na kikosi chake. Ufaransa imeonyesha kiwango cha kipekee, nasi pia tumefanya hivyo. Mechi iko wazi kwa pande zote na itahitaji wachezaji wenye nguvu na ari mpya. Sasa kwa kuwa tumefika hapa, tutapambana kwa kila kitu tulichonacho,” alisema kocha huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.