Kocha wa Uhispania, Luis de la Fuente, amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa hatua ya 32 Bora ya michuano ya Dunia dhidi ya Austria, huku Lamine Yamal, Víctor Muñoz na Yeremy Pino wote wakiwa fiti na tayari kucheza.
De la Fuente amesema anaona maendeleo makubwa ndani ya kikosi chake baada ya mwanzo usioridhisha wa mashindano, ambapo Uhispania ilitoa sare dhidi ya Cape Verde, ikashinda kwa tabu dhidi ya Uruguay, kabla ya kuonyesha kiwango bora katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Saudi Arabia.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Ninachokiona wiki hii ni kwamba timu inaanza kutambua maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa kutokana na matokeo yetu ya awali,” alisema De la Fuente.
Kocha huyo alieleza kuwa Lamine Yamal sasa yuko tayari kucheza dakika nyingi zaidi baada ya kupona majeraha ya msuli wa nyuma wa paja, huku Yeremy Pino akirejea baada ya kupona jeraha la bega na Víctor Muñoz akiwa fiti tena kufuatia matatizo ya misuli yaliyomuweka nje kwa muda.
“Ninafurahia matarajio makubwa yaliyowekwa kwetu. Watu wanatarajia mengi kutoka kwetu, na jukumu letu ni kuyatimiza matarajio hayo,” alisema De la Fuente, ambaye pia alithibitisha kuwa tayari ameshachagua kikosi kitakachoanza dhidi ya Austria, lakini akakataa kuweka wazi majina ya wachezaji wake.


