Kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Luis de la Fuente, amesema amerejea kutazama tena mchezo wa fainali ya UEFA Nations League 2025 waliopoteza dhidi ya Ureno ili kupata mbinu zitakazowasaidia kulipiza kisasi katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Dunia dhidi ya wapinzani hao utakaochezwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Dallas.
De la Fuente alisema analenga kuifahamu vizuri timu ya Ureno kwa kuchambua nguvu na udhaifu wake, akiamini kuwa maelezo madogo yatakuwa na mchango mkubwa katika kuamua mshindi wa mchezo huo muhimu wa hatua za mtoano.
“Nimetazama tena mchezo huo kwa sababu tunataka kujikumbusha sifa za wapinzani wetu. Maelezo madogo yataamua matokeo ya kesho, hivyo kadri tunavyowafahamu vizuri ndivyo tutakavyokuwa katika nafasi nzuri zaidi. Tunajua wana nguvu nyingi, lakini kila timu pia ina udhaifu wake,” alisema De la Fuente.
Akizungumzia mshambuliaji mkongwe wa Ureno, Cristiano Ronaldo, kocha huyo alimwelezea kuwa ni mchezaji wa kipekee ambaye ana uwezo wa kubadili matokeo ya mchezo kwa muda mfupi, huku akikiri angependelea kutomwona akicheza lakini anaamini atakuwepo uwanjani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Cristiano ni gwiji wa soka. Lazima umuangalie kwa makini kwa sababu anaweza kubadili mchezo wakati wowote. Ana ubora na kiwango cha juu, hivyo ni mchezaji ambaye anaweza kuamua matokeo. Kwa kweli ningependa asicheze, lakini naamini atakuwepo,” alisema De la Fuente.
Kocha huyo pia alisema anajivunia kuona timu yake ikilinganishwa na kikosi cha Hispania kilichotwaa michuano ya Dunia mwaka 2010, akisisitiza kuwa wachezaji wake bado wana safari ndefu mbele yao na wana uwezo wa kupigania mataji makubwa katika miaka ijayo.


