De Zerbi Amtilia Shaka Kulusevski, Asema Kombe La Dunia Si Rahisi Hivyo

Kocha wa Tottenham, Roberto De Zerbi, ameibua mjadala mkubwa baada ya kuonyesha mashaka kuhusu uwezo wa Dejan Kulusevski kucheza Kombe la Dunia lijalo akiwa na Sweden. Ingawa nyota huyo ameendelea kuonyesha matumaini makubwa ya kurejea kwa wakati, kocha wake anaona safari hiyo inaweza kuwa ngumu kutokana na muda mrefu aliokaa nje ya uwanja.

De Zerbi Amtilia Shaka Kulusevski, Asema Kombe La Dunia Si Rahisi Hivyo

Kulusevski hajacheza tangu Mei 2025 baada ya kusumbuliwa na majeraha ya goti yaliyochukua muda mrefu kupona. Safari yake ya kurejea imekuwa ngumu, huku akilazimika hata kufanyiwa matibabu mengine madogo ili kuhakikisha anapona vizuri. Hali hiyo imeweka mashabiki wa Sweden kwenye wasiwasi mkubwa kuelekea mashindano hayo makubwa duniani.

Akizungumzia hali ya mchezaji huyo, De Zerbi alisema ni vigumu kuelewa namna ambavyo mchezaji ambaye hajacheza msimu mzima anaweza kuwa tayari kwa kiwango cha Kombe la Dunia. Hata hivyo, alithibitisha kuwa bado wana mawasiliano mazuri na anatarajia Kulusevski kurejea Tottenham wiki zijazo kuendelea na mazoezi ya kujiweka sawa.

De Zerbi Amtilia Shaka Kulusevski, Asema Kombe La Dunia Si Rahisi Hivyo

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Lakini kwa upande wa Kulusevski mwenyewe, matumaini bado yapo juu. Nyota huyo amesema anaamini uwezo wake binafsi unaweza kufanya jambo ambalo wengi hawaamini linawezekana. Ameweka wazi kuwa ndoto yake si tu kushiriki Kombe la Dunia, bali kuifanya Sweden iwe timu inayoheshimika dhidi ya mataifa makubwa kama Brazil na Ufaransa.

De Zerbi Amtilia Shaka Kulusevski, Asema Kombe La Dunia Si Rahisi Hivyo

Wakati huo huo, De Zerbi aliwatoa hofu mashabiki kuhusu Richarlison baada ya mshambuliaji huyo kukosa mazoezi. Kocha huyo alisema tatizo si jeraha kubwa bali ni uchovu uliotokana na juhudi kubwa alizoonyesha dhidi ya Aston Villa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.