Kocha wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi, amesema wachezaji wake wanapaswa kuonyesha damu, tabia na moyo wa kupambana katika mchezo wao wa mwisho wa kuwania kubaki kwenye Ligi Kuu England dhidi ya Everton Jumapili hii.
De Zerbi alipuuza mjadala kuhusu nahodha wa timu hiyo, Cristian Romero, ambaye ameondoka kwenda Argentina kwa ajili ya kuendelea na matibabu ya goti akiwa na madaktari wa timu ya taifa kabla ya Kombe la Dunia mwezi ujao, huku Spurs wakibaki pointi mbili tu juu ya eneo la kushuka daraja.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Nikiwa naye ameonyesha mara zote hamu ya kubaki nasi. Ameumia, mimi si mjinga. Sidhani kama uwepo wake uwanjani au kutokuwepo unaweza kubadili chochote. Hatuna muda wa kupoteza nguvu kufikiria mambo mengine, tunapaswa kuelekeza akili kwenye mchezo,” alisema De Zerbi.
Spurs wanahitaji sare pekee dhidi ya Everton ili kujihakikishia kubaki Ligi Kuu, kutokana na kuwa na tofauti nzuri ya mabao dhidi ya West Ham United walio nafasi ya 18.
“Tunapaswa kucheza kwa damu, tabia na roho ya mapambano kwa sababu huu ni mchezo wa fainali,” alisema De Zerbi huku akikumbushia ubingwa wa Europa League waliouchukua Spurs msimu uliopita chini ya kocha wa zamani Ange Postecoglou.
“Baada ya kesho hakuna kombe wala bonus, kuna jambo muhimu zaidi — mustakabali na historia ya klabu. Fahari ya wachezaji na heshima ya kila mmoja wetu.”
Katika taarifa nyingine nzuri kwa Spurs, mshambuliaji Dominic Solanke amerejea baada ya kuukosa uwanja kwa karibu mwezi mmoja kutokana na majeraha ya misuli ya nyuma ya paja.
De Zerbi amesema Solanke yupo tayari kucheza lakini bado wataamua kama ataanza kikosi cha kwanza. Pia beki Djed Spence, aliyepata jeraha la kuvunjika taya dhidi ya Chelsea, anatarajiwa kuwepo kwenye mchezo huo muhimu.
“Kuwa chini ya presha ni jambo zuri. Inategemea kama unaweza kubaki imara, mwenye mawazo chanya na mwenye utulivu. Michezo kama hii inaweza kukufanya kuwa kocha bora, mchezaji bora na mtu bora zaidi,” aliongeza De Zerbi.


