Kocha wa Tottenham Hotspur F.C., Roberto De Zerbi, amewataka wachezaji wake kutumia kejeli na presha kutoka kwa wapinzani wao kama nguvu ya kupambana na hatari ya kushuka daraja katika Premier League.
Tottenham kwa sasa ipo juu ya eneo la kushuka daraja kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya West Ham United F.C., huku ikipewa jukumu la kutafuta angalau pointi mbili katika michezo yake miwili iliyobaki ili kuhakikisha inabaki ligi kuu msimu ujao.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, pointi moja inaweza kutosha kutokana na Spurs kuwa na tofauti kubwa ya mabao dhidi ya wapinzani wao wa karibu. Tottenham ambayo mara ya mwisho kushuka daraja ilikuwa mwaka 1977, itavaana na mahasimu wao wa London Chelsea F.C. Jumanne usiku.
Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu, De Zerbi alisema timu yake inapaswa kuigeuza presha hiyo kuwa motisha kubwa ya kupambana hadi mwisho wa msimu.
“Tunapaswa kutafuta motisha mpya kupitia presha hii. Kama kila mtu anataka Tottenham ishuke daraja, basi hiyo ni motisha kubwa kwangu na naamini pia kwa wachezaji wangu,” alisema De Zerbi.
Kocha huyo raia wa Italia alisema ushindani wa soka ni sehemu ya mchezo na Spurs wanapaswa kufurahia changamoto hiyo huku wakipambana kupata ushindi kwenye viwanja vya wapinzani wao.
“Tunapaswa kukubali kuwa soka linapendeza kwa sababu ya ushindani. Ni jambo zuri kujifikiria tukisherehekea ushindi kwenye uwanja wao,” aliongeza.
Tottenham itamaliza msimu kwa mchezo wa nyumbani dhidi ya Everton F.C. siku ya Jumapili, huku West Ham ikiwa imebakiza mchezo mmoja pekee dhidi ya Leeds United F.C..


