Beki wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Zeno Debast, amesema kikosi chao kipo tayari kuikabili Senegal katika hatua ya 32 bora ya mashindano ya Dunia, licha ya kutotarajia kukutana na wawakilishi hao wa Afrika. Ubelgiji ilijihakikishia nafasi ya kuongoza Kundi G baada ya kuibuka na ushindi mkubwa wa mabao 5-1 dhidi ya New Zealand.
Awali, Ubelgiji ilitarajiwa kukutana na Korea Kusini, lakini ushindi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya Uzbekistan ulibadilisha mwelekeo wa ratiba na kuifanya Senegal kuwa mpinzani wao rasmi. Akizungumzia hali hiyo, Debast alisema, “Ilikuwa hisia ya ajabu kidogo, lakini sasa tunajua tunacheza dhidi ya Senegal na tuna takribani siku tatu za kujiandaa kwa mchezo huo.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Beki huyo alieleza kuwa Senegal ni timu yenye ubora mkubwa na haitapaswa kubezwa. “Senegal ni timu nzuri sana. Wana nguvu kimwili, wana mbinu nzuri na walitwaa Kombe la Mataifa ya Afrika. Ninaamini utakuwa mchezo mzuri kwa sababu nasi tuna ubora wetu. Tukiendelea kucheza kama tulivyofanya katika mechi iliyopita, tutakuwa na nafasi nzuri,” alisema.
Debast bado hajacheza katika mashindano hayo kutokana na majeraha ya mguu, lakini amesema maendeleo ya afya yake yanaendelea vizuri. Alifanyiwa uchunguzi wa MRI hivi karibuni ambao ulionyesha kuwa ameendelea kupona kama ilivyopangwa.
“Matokeo ya uchunguzi yalikuwa mazuri na kila kitu kinaenda kama tulivyotarajia. Najisikia vizuri na leo nimeanza kushiriki sehemu ya mazoezi ya timu, hivyo nina matumaini makubwa ya kurejea uwanjani hivi karibuni,” alisema Debast huku akiongeza kuwa yupo tayari kusaidia Ubelgiji endapo atapewa nafasi katika hatua ya mtoano.


