Ulikuwa ni mchezo mgumu kwa pande zote mbili kulingana na uhitaji wa matokeo na umihimu wa mchezo wenyewe, ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara ambapo ulimalizika kwa Simba kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya walima miwa wa Kagera (Kagera Sugar).

DEJAN, Dejan Georgijevic: Gari Limewaka Atuma Salamu kwa Wapinzani., Meridianbet

Stori sio Simba kushinda, bali shangwe na habari ya mjini kwa sasa ni goli la Mshambuliaji wa lunyasi raia wa Serbia Dejan Georgijevic, kwa siku za hivi karibuni amekuwa maarufu sana kulingana asili yake ya uzungu ambaye mashabiki wengi wamekuwa wakimuita “Mzungu”.

Mara baada ya mechi kumalizika, Dejan alipata nafasi ya kufanyiwa mahojiano na Azam Media na kuzungumzia goli lake hilo la kwanza linampa hali gani ambapo alisema kuwa, yeye binafsi hali ya kutokufunga haijamfanya awe na mawazo sana kwani ndio kwanza amecheza mechi mbili za ligi, na hivyo alikuwa anafanya mazoezi akiongeza kuwa yeye anaamini katika uwezo wake wa ufungaji huku akiwataka mashabiki na wanasimba watarajie mambo makubwa.

DEJAN, Dejan Georgijevic: Gari Limewaka Atuma Salamu kwa Wapinzani., Meridianbet

Akizungumzia juu ya mashabiki ambao walikuwa wanahamu ya kumuona akifunga amesema kuwa

“Nimepokea jumbe nyingi sana kutoka kwa mashabiki, nina furaha kwa goli hili na nawashukru sana mashabiki kwa uvumilivu wao na kwa jinsi walivyonikaribisha”

Kwa upande wa Kagera Sugar Mchezaji Abdallah Seseme, amesema kuwa walicheza na wakubwa ingawa na wao walikuwa na mipango yao ambayo, haikufanikiwa kutokana na ukubwa wa Klabu ya Simba.

DEJAN, Dejan Georgijevic: Gari Limewaka Atuma Salamu kwa Wapinzani., Meridianbet

Sasa baada ya michezo ya jana kumalizika, msimamo wa ligi kuu unaonesha Simba wanaongoza kwa utofauti wa magoli ya kufanga kwani wana alama 6, sawa na watani zao Yanga huku Simba akiwa na jumla ya magoli 5, na hajaruhusu goli hata moja huku Yanga akiwa na 4 ya kufunga na 1 la kufungwa, wakifuatiwa na Namungo mwenye alama 4 kibindoni.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa