Mchezaji wa Barcelona Ousmane Dembele amekabuliana na klabu hiyo kusaini mkataba wa miaka miwili kwa kukubali kupunguzwa kwa mshahara wake.

Dembele Aongeza Miaka Miwili na Barcelona

Taarifa zinadai kwamba Dembele atakatwa mshahara wake kwa alsimia 40% kutoka kwenye mshara wake wa uliyopita.

Dembele alianza mazoezi na kikosi kizima cha Barcelona na tayari amehudhuria mara mbili kwenye mazoezi na ataweza kusafiri na timu siku ya Jumamosi kwaajili ya michezo ya kabla ya msimu nchini Marekani.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alikuwa akihuisishwa kuondoka Camp Nou na Chelsea ndiyo klabu aliyokuwa akihusishwa lakini Dembele hakuwa na dhamira ya kuondoka klabuni hapo kwa sasa.

Kocha wa Barca Xavi Hernandez anamtazama Dembele kama mchezaji muhimu kwenye timu yake hivyo Dembele kusalia ni habari njema kwake.


BASHIRI MICHEZO MBALIMBALI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa