Deschamps Ampongeza Mbappe Baada ya Kuipeleka Ufaransa Nusu Fainali

Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps, amempongeza mshambuliaji wake Kylian Mbappe baada ya kufunga bao lake la nane katika michuano ya Dunia 2026 na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Morocco, matokeo yaliyoihakikishia Ufaransa tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali kwa mara ya tatu mfululizo.

Deschamps Ampongeza Mbappe Baada ya Kuipeleka Ufaransa Nusu FainaliMbappe alifunga bao hilo dakika ya 60 baada ya awali kukosa penalti iliyookolewa na kipa wa Morocco, huku Ousmane Dembele akifunga bao la pili lililohitimisha ushindi wa Ufaransa. Akizungumza baada ya mchezo, Deschamps alisema mchezaji huyo huwa hapotezi kujiamini hata anapokutana na changamoto. Linapokuja suala la Kylian hakuna tatizo. Huwahi kuwa na mashaka na uwezo wake, hata baada ya kukosa penalti aliendelea kuamini na baadaye akafunga,” alisema kocha huyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Deschamps amesema kufuzu nusu fainali kwa mara ya tatu mfululizo ni mafanikio makubwa ambayo hayapaswi kuchukuliwa kuwa ya kawaida. Inaonekana kama jambo la kawaida, lakini si rahisi kulifikia. Tunayo timu yenye wachezaji bora na hilo limetusaidia kufika hapa, ingawa leo tulipoteza nafasi kadhaa ambazo tulipaswa kuzitumia vizuri zaidi,” alieleza.

Deschamps Ampongeza Mbappe Baada ya Kuipeleka Ufaransa Nusu FainaliKocha huyo amesema sasa kikosi chake kitaelekeza nguvu kwenye maandalizi ya mchezo wa nusu fainali, ambapo kitapambana na mshindi wa robo fainali kati ya Hispania na Ubelgiji. “Tupo mahali tulipotaka kufika. Sasa tutapumzika vizuri kisha tutamsubiri mpinzani wetu atakayejulikana baada ya mchezo wa kesho,” alisema.

Deschamps Ampongeza Mbappe Baada ya Kuipeleka Ufaransa Nusu FainaliDeschamps pia alifafanua sababu ya kumtoa Mbappe kipindi cha pili, akisema mshambuliaji huyo alipata maumivu madogo ya kifundo cha mguu wakati wa mchezo. Tuliamua kumtoa baada ya kupata maumivu kwenye kifundo cha mguu. Tunaamini si tatizo kubwa, lakini tuliona ni vyema kumlinda kwa ajili ya michezo ijayo,” alihitimisha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.