Kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa imekumbwa na pigo kubwa baada ya kocha mkuu Didier Deschamps kufiwa na mama yake mzazi, Marie Borda, hali iliyomlazimu kuondoka mara moja kambini ili kwenda kuungana na familia yake nchini Ufaransa.
Shirikisho la Soka la Ufaransa limethibitisha taarifa hiyo likisema: “Kocha wa timu ya taifa alihuzunishwa sana kujua asubuhi ya leo kuhusu kifo cha mamake.” Taarifa hiyo imeeleza kuwa Deschamps amechukua likizo ya muda kushughulikia msiba huo wa kifamilia.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Deschamps hatakuwepo katika mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Norway utakaopigwa Juni 26, 2026, huku akiamua kukabidhi majukumu kwa msaidizi wake wa kwanza Guy Stéphan ili kuongoza kikosi wakati wa kutokuwepo kwake.
Katika makubaliano na uongozi wa shirikisho, imeelezwa kuwa: “Kwa makubaliano na Rais wa FFF Philippe Diallo, Didier Deschamps amemkabidhi msaidizi wake Guy Stephan jukumu la kuongoza kikosi hadi atakaporejea,” huku uamuzi huo ukilenga kuhakikisha maandalizi ya timu hayaathiriki.
Deschamps, mwenye umri wa miaka 57, ni mmoja wa makocha waliodumu kwa muda mrefu na wenye mafanikio makubwa katika historia ya Ufaransa, akiwa ameiongoza timu hiyo tangu mwaka 2012, na sasa anatarajiwa kurejea baada ya kumaliza majukumu ya kifamilia.


