Deschamps Yupo Ufaransa Mpaka 2026

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amekubali kusaini mkataba wa kusalia ndani ya timu ya taifa ya Ufaransa kocha huyo ataendelea kuitumikia timu hiyo mpaka mwaka 2026.

Deschamps ambaye mkataba wake ulikua unamalizika baada ya michuano ya kombe la dunia nchini Qatar mwezi uliopita, Lakini kwa wiki kadhaa amekua kwenye mazungumzo na shirikisho la soka la Ufaransa (FFF) na kukubali kusaini mkataba utakaomuweka kwenye timu hiyo mpaka mwaka 2026.deschampsKocha Deschamps amefanikiwa kuiongoza timu ya taifa ya Ufaransa kwenye fainali nne mpaka sasa hivi huku akifanikiwa kushinda fainali mbili kati ya hizo. Fainali ya Euro mwaka 2016 akipoteza mbele ya Ureno 2018 fainali ya kombe la dunia akishinda mbele ya Croatia, Fainali ya Uefa nations League mwaka 2021 akishinda mbele ya Hispania, Fainali  ya kombe la dunia dhidi ya Argentina mwaka 2022 akipoteza kwenye matuta.

Shirikisho la soka nchini Ufaransa (FFF) limetangaza mapema leo kua wamekubaliana pande zote kua kocha huyo aendelee kuhudumu taifa hilo mpaka mwaka 2026. Na hii inamaanisha kocha huyo ataitumikia timu hiyo mpaka fainali za kombe la dunia 2026 zitakazofanyika Marekani,Canada, na Mexico.deschampsTaarifa za mwanzo zilikua zinaeleza kua gwiji wa zamani wa taifa hilo na kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane ataichukua timu hiyo baada ya michuano ya kombe la dunia nchini Qatar, Lakini ni wazi sasa kua Deschamps bado yupoyupo sana ndani ya Ufaransa.

Acha ujumbe