Angel Di Maria, Neymar,Leandro Paredes na Keylor Navas wamejumuishwa katika kikosi cha Paris Saint-Germain kwa mchezo wa Jumapili wa Ligue 1 dhidi ya Marseille baada ya kumaliza siku za kukaa Karantini.

Wachezaji hao waliukosa mchezo wa ufunguzi wa Ligue 1 msimu 2020-21 dhidi ya Lens mchezo ambao PSG ilipoteza kwa 1-0 siku ya Alhamisi baada ya kuwa na maambukizi ya COVID-19.

Majibu ya vipimo kwa Di Maria na wenziye

Lakini,wachezaji wote wanne wamepimwa na vipimo vilionesha hawana COVID-19 tena na kocha Thomas Tuchel kuelekea mchezo huo alisema kwamba wachezaji hao wamejumuishwa katika kikosi na watashiriki katika mazoezi.


Di Maria na Neymar Warejea Kikosini Baada.
Neymar na Di Maria

Na sasa imethibitika kwamba washambuliaji wawili Neymar na Di Maria pamoja na kiungo Paredes na golikipa Navas ambaye ni chaguo la kwanza, watakuwa sehemu ya kikosi cha PSG chenye watu 21 katika dimba Classique.

Kylian Mbappe, Mauro Icardi na Marquinhos majibu yao yalionesha bado wana COVID-19 baada ya kupimwa tena wiki iliyopita na watakosa tena mchezo wa pili wa Ligue 1.

Akiongea kabla ya mechi, Tuchel aliulizwa kwanini mchezo mmoja wa mapema katika ratiba ya Ligue 1 ulisogezwa mbele.

“Nimeshangazwa kwa mechi muhimu kama ile kuwekwa ya tatu,” Aliwambia maripota.

“Nadhani gemu kama ile ilitakiwa iwekwe Oktoba au Novemba wakati timu zote zikiwa zimepata ladha ya ligi, binafsi sijaelewa kabisa maamuzi yaliyofanywa.


SHINDA NA MERIDIANBET!

Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.

Cheza Sasa.


43 MAONI

  1. Nadhani gemu kama ile ilitakiwa iwekwe Oktoba au Novemba wakati timu zote zikiwa zimepata ladha ya ligi, binafsi sijaelewa kabisa maamuzi yaliyofanywa.#meridianbet

  2. Habari njema kwa PSG maana sasa klabu itachangamka maaan majamaa sio wa mchezo kabisa mechi hii dhidi ya Marseille hawatowaacha salama

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa