Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amesema kwamba jina la uwanja wa klabu linatakiwa libadilishwe kwa heshima ya kumenzi mkongwe Diego Maradona baada ya kufariki siku ya Jumatano.
Dimba la Napoli Kupewa Jina la  San-Paolo Maradona.
Nje ya Dimba la Stadio San-Paolo.

Maradona ni mchezaji bora wa dunia wa muda wote, amefariki akiwa na umri wa miaka 60 baada ya kugundulika kuwa na shambulio la moyo, chama cha mpira nchini Argentina (AFA) kilithibitisha katikati ya wiki.

Mshindi huyo wa kombe la dunia akiwa na Argentina alifurahia mafanikio mbalimbali akiwa Naples,ambako aliiongoza Napoli kutwaa taji la Serie A mwaka 1986-87 na 1989-90.

Kama mashabiki wa Napoli na wananchi wa Naples wameshitushwa na kifo cha mkongwe Maradona na Rais wa De Laurentiis amesema dimba la Stadio San Paolo linatakiwa libadilishwe jina na kuitwa jina la gwiji huyo kama ishara ya kuheshimu mchango wake.

“Itakua wazo zuri kulibadili jina la uwanja na kuuita San Paolo-Maradona ni jambo ambalo tunaweza tukalifikiria,” De Laurentiis aliiambia RMC Sport.

Meya wa jiji Luigi de Magistris pia alitweet: “Acha tuite dimba la San Paolo, Diego Armando Maradona!!!”

Gennaro Gatuso na timu yake ya Napoli wataiongoza Rijeka katika dimba la San Paolo siku ya Alhamisi kwenye michuano ya Europa League katika kundi F.

Napoli wapo nafasi ya pili katika jedwali la Europa League wakiwa nyuma ya AZ Alkmaar kwa tofauti ya magoli.

“Ningependa kuona sura ya Maradona ndani ya uwanja wakati wote wa mchezo siku ya Alhamisi,” alisema De Laurentiis.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

20 MAONI

  1. Utakuwa uamuzi sahihi kwa Napoli na Mashabiki kwa ujumla maana bila Diego Maradona Napoli isingechukua ubingwa wa ligi ya Italy na ndiko alikoanza tatizo la kutumia madawa ya kulevya

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa