DR Congo ina vilabu viwili vikubwa [AS Vita na TP Mazembe] ambavyo vitatikisa soka la Afrika! Lakini ukiangalia wachezaji wanaoanza kwenye kikosi cha timu ya taifa hakuna mchezaji wa AS Vita wala Mazembe. Dakika 90 zinamalizika hakuna mchezaji aliyecheza kutoka Vita wala Mazembe!
Hapa inabidi ujiulize, wachezaji wanaocheza vilabu vikubwa vya DR Congo kwa nini hawapati nafasi kwenye timu yao ya taifa?
Wakati timu ya taifa inajiandaa na mchezo dhidi ya Tanzania kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia, Ligi ya DR Congo haikusimama…ilikuwa inaendelea kama kawaida.
Shughuli za mpira nchini DR Congo zilikuwa zinaendelea kama kawaida, timu ya taifa haikuathiri chcochote kiendelea lakini sisi bado tunasimamisha kila kitu ili kupisha timu ya taifa kwa sababu tunategemea wachezaji wa ndani.

Kwenye vilabu vyetu vya Simba na Yanga ambavyo ndio tunategemea na imekuwa utamaduni wetu vilabu hivyo vitoe wachezaji wa kuibeba Taifa Stars, kwenye kikosi cha jana kuna wachezaji [Kennedy Juma, Mzamiru Yassin] ukiangalia ckaenye mechi 5 zilizopita za Simba hawajapata nafasi ya kutosha!
Wachezaji hao sio kwamba walikuwa na majeraha lakini wanaweka benchi na wachezaji wakigeni lakini kwenye timu ya taifa tunawategemea tena kwenye mechi ya kutoa maamuzi!
Mzamiru na Kennedy sio wachezaji wabaya hata kidogo, hawa nimetolea mfano lakini wanawakilisha wachezaji wengi lakini jiulize kwa nini kwenye klabu yao hawapati nafasi? Ukipata jibu pia ni sehemu ya fundisho.
Mzamiru na Kennedy wanakosa nafasi ya kutosha Simba kwa sababu nafasi zao zimezibwa na wageni [Inonga, Onyango, Wawa] Kennedy anapata wapi nafasi? [Lwanga, Kanoute, Bwalya] wanamuweka nje Mzamiru.
Tusisumbuke na matokeo ila matokeo yatupe kitu cha kujifunza ili wakati mwingine tuweze kutatua matokeo ili twende mbele.
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?