Golden State Warriors wanaonekana kuingia kwenye kharakati za kutafuta mrithi wa wa nyota mkongwe Draymond Green. Licha ya kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya klabu kwa miaka mingi, umri wa Green, sasa akiwa na miaka 36, umeanza kuifanya timu hiyo kuangalia mustakabali mpya kupitia NBA Draft.

Majina mawili ya vijana yanatajwa kwa nguvu kama chaguo la Warriors katika pick yao ya 11, Yaxel Lendeborg na Morez Johnson Jr. Wachezaji hao wawili, ambao wote walicheza Michigan na kushinda ubingwa pamoja, wanaonekana kuwa na uwezo wa kuleta nguvu mpya katika safu ya mbele ya Golden State.
Lendeborg ndiye anayezungumziwa zaidi baada ya kufanya mazoezi ya kuvutia na Warriors wiki hii. Mashabiki wengi wametaka timu yao imchague kutokana na uwezo wake wa ulinzi wa kubadilika na pia uwezo wa kusaidia kushambulia kama mchezaji wa pili anayeanzisha mashambulizi. Hata yeye mwenyewe amekiri kuwa ana sifa zinazofanana na Draymond Green, hasa katika upande wa ulinzi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, usajili wake unaweza kuleta changamoto ya kiufundi iwapo atacheza sambamba na Green, kwani wote wana sifa zinazofanana za nafasi na mtindo wa mchezo. Hii ina maana kocha Steve Kerr atalazimika kufanya maamuzi magumu kuhusu jinsi ya kutumia kikosi chake iwapo atamsajili mchezaji huyo kijana.

Kwa upande mwingine, Morez Johnson Jr. amekuwa akivutia na anaaminika kuwa mmoja wa mabeki bora wa baadaye katika draft hii. Wachambuzi wengi wanaona anaweza kuwa toleo la baadaye la Draymond Green kutokana na uwezo wake wa ulinzi na nguvu uwanjani.



