Dybala Afunguka Hatma Yake Roma Kabla ya Mchezo Dhidi ya Lazio

Mshambuliaji wa AS Roma, Paulo Dybala amesema mchezo wa dabi dhidi ya Lazio unaotarajiwa kuchezwa Jumapili huenda ukawa wa mwisho kwake kucheza mbele ya mashabiki wa Roma katika Uwanja wa Olimpico.

Dybala Afunguka Hatma Yake Roma Kabla ya Mchezo Dhidi ya LazioNyota huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 32 alisema bado hajapata mawasiliano yoyote kutoka kwa uongozi wa Roma kuhusu mustakabali wake klabuni hapo, jambo lililoibua maswali kuhusu hatma yake mwishoni mwa msimu huu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Ukweli ni kwamba hata mimi ningependa kujua kinachoendelea, lakini klabu bado haijanifuata kuzungumza nami,” alisema Dybala katika mahojiano. “Mkataba wangu unaonyesha kuwa dabi hii huenda ikawa mechi yangu ya mwisho mbele ya mashabiki wa Roma, lakini tutaona nini kitatokea mwishoni mwa msimu.”

Dybala Afunguka Hatma Yake Roma Kabla ya Mchezo Dhidi ya LazioDybala ambaye aliwahi kuitumikia Juventus kwa miaka saba kabla ya kujiunga na Roma mwaka 2022, ameandamwa na majeraha msimu huu ikiwemo matatizo ya misuli ya nyuma ya paja pamoja na kufanyiwa upasuaji wa goti mwezi Machi, hali iliyomfanya kukosa karibu miezi minne ya msimu.

Dybala Afunguka Hatma Yake Roma Kabla ya Mchezo Dhidi ya LazioLicha ya changamoto hizo, Dybala alitoa pasi ya bao katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Parma uliowafanya Roma kufikisha alama sawa na AC Milan waliopo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Serie A.

Dybala Afunguka Hatma Yake Roma Kabla ya Mchezo Dhidi ya Lazio“Tumekuwa tukionyesha dhamira na hamu kubwa ya kuhakikisha tunapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Tunajua haitegemei sisi pekee, lakini tutaendelea kupambana hadi mwisho,” alisema Dybala kuhusu mbio za kumaliza katika nafasi za juu msimu huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.