Mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan ya nchini Italia raia wa Bosnia Edin Dzeko amesema klabu yake inaweza kuwafikia vinara Napoli ambao wanaongoza ligi kuu ya Italia.

Mshambuliaji Dzeko amekiri kua klabu yake ya Inter Milan inahitaji kuongeza kasi na kufanya kazi kubwa ili kuweza kuwafikia vijana wa Luiciano Spaletti vinara klabu ya Napoli ambao wamekua na msimu bora.dzekoKlabu ya Inter Milan ambayo ilibeba ubingwa msimu mmoja uliopita kabla ya majirani zao klabu ya soka ya Ac Milan kubeba ubingwa msimu uliomalizika,Huku klabu hiyo ikiwa imeanza msimu huu vibaya baada ya kupoteza michezo mitano ya awali kati ya 15 waliyocheza kabla ya mapumziko ya kombe la dunia.

Mshambuliaji wa Edin Dzeko anaelewa ugumu ambao wako nao kurudisha ubora wao baada ya ligi kurejea mwezi Januari mwakani,Huku mshambuliaji huyo akisisitiza kua wanahitaji kufanya kazi ya ziada ili kuwafikia klabu ya Napoli.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa