Mshambuliaji chipukizi wa Brazil, Endrick, amesema ameridhika na nafasi yake ndani ya kikosi cha timu ya taifa katika michuano ya Dunia, licha ya kutopata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza mara kwa mara. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 amesema ana imani kubwa na maamuzi ya kocha Carlo Ancelotti kuelekea mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Norway.
Endrick, ambaye pia anachezea Real Madrid chini ya Ancelotti, hajacheza mechi ya kwanza dhidi ya Morocco, lakini alipata dakika 26 dhidi ya Haiti, akaingia mwishoni dhidi ya Scotland na kucheza dakika 45 dhidi ya Japan. Licha ya mashabiki wengi kutaka apewe nafasi kubwa zaidi, amesema kocha wake huweka maslahi ya timu mbele kuliko ya mchezaji mmoja mmoja.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Kocha hafanyi kilicho bora kwa Endrick, anafanya kilicho bora kwa Brazil. Ninaamini maamuzi yake kwa sababu anajua nini kinafaa kwa timu, na ninapopewa maelekezo natekeleza bila kusita,” amesema Endrick.
Nyota huyo amesema hana presha kuhusu muda anaopata uwanjani na anaamini nafasi yake itafika kwa wakati sahihi. Ameeleza kuwa siri ya utulivu wake ni kuwa na imani kwa Mungu na kuendelea kufanya kazi kwa bidii kila siku.
“Ninalala kwa amani kabisa. Kabla ya kulala husali na kumkabidhi Mungu kila jambo. Kuwa sehemu ya kikosi cha Brazil katika michuano ya Dunia tayari ni mafanikio makubwa kwangu, na nitakuwa tayari pindi nafasi yangu itakapofika,” amesema Endrick. Pia amemsifu Ancelotti kama mmoja wa makocha bora duniani, akisema uzoefu wa kufanya naye kazi Real Madrid umemjengea kujiamini na kumsaidia kuelewa falsafa yake ya soka.


