Nahodha wa England, Harry Kane, amesema anajivunia moyo wa kupambana ulioonyeshwa na timu yake baada ya kuibuka na ushindi mgumu dhidi ya Mexico katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Dunia 2026 uliopigwa kwenye Uwanja wa Estadio Azteca.
England ilijikuta kwenye wakati mgumu baada ya beki Jarell Quansah kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kucheza faulo ya hatari, hali iliyowalazimu Three Lions kucheza kwa idadi pungufu kwa sehemu kubwa ya mchezo. Licha ya changamoto hiyo, walifanikiwa kusimama imara na kutafuta ushindi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kiungo Jude Bellingham aliifungia England mabao mawili ndani ya sekunde 98 kipindi cha kwanza kabla ya kuigharimu timu yake kwa kusababisha penalti iliyotolewa baada ya mwamuzi kupitia picha za VAR. Baadaye, Harry Kane aliifungia England bao la penalti lililowapa nafasi ya kuendelea na ushindi huo muhimu.
“Ilikuwa mechi ya kichaa. Tulilazimika kupambana na kutafuta njia ya kushinda. Nimekuwa nikiimba sana kusherehekea kiasi kwamba siwezi hata kuzungumza vizuri. Kila kitu kilionekana kuwa dhidi yetu, lakini tulipata njia ya kushinda,” alisema Kane.
Akizungumzia maamuzi ya mwamuzi, Kane alisema aliamini aliuwahi mpira kabla ya tukio lililozaa penalti, lakini akasisitiza kuwa kilicho muhimu zaidi ni ushindi. “Nilidhani nilikuwa nimeuwahi mpira kwanza. Mwamuzi alitoa maamuzi mengi yaliyokuwa dhidi yetu, lakini mwisho wa siku haikuwa na maana kwa sababu tumeshinda, na hilo ndilo linalonifurahisha,” aliongeza Kane.


