Enzo Fernandez Arejea Chelsea, Tayari Kuivaa Man United

Kocha wa Chelsea FC, Liam Rosenior, amethibitisha kuwa kiungo Enzo Fernandez amerejea kwenye mazoezi kamili na yupo tayari kuchaguliwa katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United utakaopigwa Jumamosi. Fernandez alikuwa ameondolewa kwenye kikosi kutokana na sababu za kinidhamu.

Enzo Fernandez Arejea Chelsea, Tayari Kuivaa Man UnitedMchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye ni mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na Argentina, alikosekana kwenye ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Port Vale katika robo fainali ya FA Cup pamoja na kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Stamford Bridge.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Awali, Fernandez alikuwa akivaa beji ya unahodha kufuatia majeraha ya Reece James, na aliwahi kutoa kauli kuhusu mustakabali wake baada ya Kombe la Dunia akieleza nia ya kuishi Madrid, jambo lililozua mjadala kabla ya kuomba radhi baadaye.

Enzo Fernandez Arejea Chelsea, Tayari Kuivaa Man UnitedAkizungumza na waandishi wa habari, Rosenior alisema, “Enzo amerejea kwenye kikosi na amekuwa akifanya mazoezi vizuri sana. Kwa sasa mambo ni ya kawaida katika suala la uchaguzi wa kikosi kwa mchezo ujao.” Kauli hiyo inaashiria kurejea kwa mchezaji huyo katika mipango ya timu.

Aliongeza kwa kusema, “Kwa upande wa mazoezi na kujituma kwake, Enzo amekuwa wa kiwango cha juu sana.” Huku akitoa taarifa za majeruhi, Rosenior alisema beki Trevoh Chalobah ameanza mazoezi lakini bado hajawa fiti kwa asilimia 100, wakati Reece James bado yupo mbali kurejea uwanjani.

Enzo Fernandez Arejea Chelsea, Tayari Kuivaa Man UnitedKwa sasa, Chelsea FC ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 48, ikiwa nyuma kwa pointi nne dhidi ya timu zilizo kwenye nafasi za kufuzu UEFA Champions League. Rosenior alisisitiza umuhimu wa kupata ushindi dhidi ya United akisema, “Tunapaswa kuzingatia kile tunachoweza kudhibiti, ambacho ni kiwango chetu cha uchezaji. Natarajia kuona kiwango kizuri Jumamosi.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.