Enzo Fernandez Kukosa Mchezo Dhidi ya Man City, Licha Ya Kuomba Msamaha

Kocha wa Chelsea, Liam Rosenior, amethibitisha kuwa kiungo Enzo Fernandez hatacheza katika mchezo muhimu wa Premier League dhidi ya Manchester City, licha ya kumuomba radhi klabu baada ya kauli tata kuhusu mustakabali wake.

Enzo Fernandez Kukosa Mchezo Dhidi ya Man City, Licha Ya Kuomba MsamahaRosenior alieleza kuwa uamuzi huo umetokana na mchezaji huyo kuvuka mipaka ya maadili ya klabu, akisema “Tulikuwa na mazungumzo mazuri. Ameomba msamaha kwangu na kwa klabu. Tutashughulikia hilo baada ya mechi kubwa ya Jumapili.” Aliongeza: “Huwezi kupitiliza adhabu kutokana na kosa. Nilifanya uamuzi, na sitaki kumzuia Enzo kuwa na maisha mazuri ya soka, lakini hatacheza Jumapili.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Chelsea inaingia kwenye mchezo huo ikiwa kwenye presha kubwa baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Newcastle United na Everton, hali iliyowashusha hadi nafasi ya sita kwenye msimamo. Kwa sasa wako pointi moja nyuma ya Liverpool na saba nyuma ya Aston Villa.

Enzo Fernandez Kukosa Mchezo Dhidi ya Man City, Licha Ya Kuomba MsamahaMbali na Fernandez, Chelsea pia itawakosa wachezaji kadhaa kutokana na majeraha akiwemo Filip Jorgensen, Levi Colwill, Reece James, Trevoh Chalobah na Jamie Gittens. Hata hivyo, Rosenior anaamini kikosi chake kina uwezo wa kufanya vizuri.

Akizungumzia mpinzani wao, Rosenior alimpongeza kocha wa City, Pep Guardiola, akisema “Ameathiri sana soka la dunia. Ni kocha wa kipekee mwenye mafanikio makubwa, lakini tunataka timu yangu ionyeshe uwezo wake Jumapili.”

Enzo Fernandez Kukosa Mchezo Dhidi ya Man City, Licha Ya Kuomba MsamahaLicha ya changamoto zote, Rosenior ameonesha imani kubwa kwa timu yake, akisema “Bila shaka tunaweza kushinda. Sisi ni timu nzuri, tumepitia kipindi kigumu lakini tumekuwa tukiwapa changamoto wapinzani wetu wote, japokuwa hatujapata matokeo tuliyotarajia.”

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.