Estevao Atoa Pigo Jingine Kwa Brazil Kuelekea Kombe La Dunia

Brazil wamepata pigo kubwa kuelekea Kombe la Dunia baada ya nyota chipukizi Estevao kuthibitishwa kuwa atakosa mashindano hayo kutokana na kuumia tena misuli ya paja. Taarifa hizo zimeibua hofu kubwa kwa mashabiki wa Seleção ambao tayari walikuwa wakihangaika na majeraha ya mastaa wengine muhimu kama Rodrygo na Eder Militao.

Estevao Atoa Pigo Jingine Kwa Brazil Kuelekea Kombe La Dunia

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Fabrizio Romano na Globoesporte, Estevao hataweza kupona kwa wakati kabla ya mashindano kuanza. Hii ni habari mbaya kwa Brazil kwani kijana huyo alikuwa kwenye kiwango cha moto, akiwa amefunga mabao matano katika mechi sita za mwisho alizoichezea timu ya taifa.

Katika kipindi ambacho safu ya ushambuliaji ya Brazil imeonekana kupoteza makali yake, Estevao alikuwa ameanza kuonekana kama tumaini jipya la mashabiki. Kasi yake, ubunifu na uwezo wa kubadilisha mchezo vilikuwa vikitoa mwanga mpya ndani ya kikosi hicho kuelekea mashindano makubwa duniani.

Estevao Atoa Pigo Jingine Kwa Brazil Kuelekea Kombe La Dunia

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Lakini huku mlango mmoja ukifungwa, mwingine unaweza kufunguka. Taarifa zinaeleza kuwa Neymar ameingizwa kwenye kikosi cha awali cha Brazil, jambo linaloongeza matumaini ya kurejea kwa staa huyo mkubwa kwenye jukwaa la dunia.

Estevao Atoa Pigo Jingine Kwa Brazil Kuelekea Kombe La Dunia

Kwa sasa, macho yote yako kwa benchi la ufundi la Brazil kuona watakavyopanga safu yao ya ushambuliaji baada ya pigo hilo kubwa. Je, Neymar atarejea kuiongoza Brazil, au Seleção wataendelea kutafuta shujaa mpya wa kubeba ndoto za taifa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.