Eze na Rice Wang’ara Arsenal Ikiitoa Leverkusen na Kutinga Robo Fainali UCL

Klabu ya Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Bayer Leverkusen mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano, na kushinda kwa jumla ya mabao 3-1.

Eze na Rice Wang’ara Arsenal Ikiitoa Leverkusen na Kutinga Robo Fainali UCLArsenal ilianza mchezo huo kwa kasi kubwa ikitengeneza nafasi kadhaa kupitia Leandro Trossard, lakini juhudi zake ziliishia kuzuiwa na kipa wa Leverkusen Janis Blaswich ambaye alikuwa imara langoni.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Bao la kwanza lilipatikana kupitia Eberechi Eze aliyefunga kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la hatari, likiwa bao lake la kwanza katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Eze na Rice Wang’ara Arsenal Ikiitoa Leverkusen na Kutinga Robo Fainali UCLArsenal waliendelea kuimarisha ushindi wao pale Declan Rice alipoongeza bao la pili kwa shuti la kuvutia lililojaa ustadi mkubwa kutoka nje ya boksi.

Licha ya Leverkusen kujaribu kusawazisha, walishindwa kupenya safu ya ulinzi ya Arsenal huku kipa David Raya akifanya kazi nzuri kuokoa michomo michache iliyolenga lango.

Eze na Rice Wang’ara Arsenal Ikiitoa Leverkusen na Kutinga Robo Fainali UCLUshindi huo unaifanya Arsenal kusonga mbele na sasa watakutana na Sporting CP katika robo fainali, huku Leverkusen wakielekeza nguvu zao kwenye kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki michuano hiyo msimu ujao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.