Kiungo wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa Fabian Ruiz amesema asingeweza kusema hapana kwa mabingwa hao wa soka la Ufaransa.

Kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Napoli ya nchini Italia ameeleza kujiunga kwake na PSG ni chaguo sahihi kwake kujiunga katika ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1.

Kiungo huyo wa kihispaniola ambaye amejiunga na timu hiyo kwea dau linalokadiriwa kufikia paundi milioni 21.

fabian ruizFabian anaeleza “Ofa ilipokuja mezani na tukaiona ni nzuri,Huwezi kukataa klabu kama Paris kwa mradi wanaoufanya kwa timu pamoja historia kwa ujumla”.


“Nilibakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wangu, Na tulianza kufanya mazungumzo na Napoli na nilivutiwa pia nafikiri lilikua chaguo zuri”.

Kiungo huyo pia anafurahia kucheza na wachezaji kama Messi,Neymar,na Mbappe.

Pia kiungo huyo ameeleza anajua ugumu atakaupata kupata nafasi kwenye kikosi cha mwalimu Christopher Galtier lakini anaeleza atapambana kuhakikisha anapata nafasi kwenye timu hiyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa